
DAR ES SALAAM; TIMU ya Fountain Gate imeingia mkataba wa miaka minne na kampuni ya michezo ya kubashiri ya PigaBet kuwa mdhamini mkuu ili kuimarisha ushindani kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa hafla hiyo Rais wa Fountain Gate, Japhet Makau alisema makubaliano hayo yana thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja na ya nalenga kuleta mapinduzi makubwa ndani ya timu hiyo inayokua kwa kasi.
“Nawashukuru PigaBet kwa uwekezaji huu mkubwa katika soka la Tanzania. Ushirikiano huu hau taisaidia tu Fountain Gate FC, bali pia utachangia ukuaji wa mpira wa miguu nchini kwa ujumla,” alisema Makau.

Aliongeza: “Ujio wao unaone sha wazi kuwa soka sasa ni chanzo muhimu cha ajira na fursa kwa vijana wetu”.
Makau alisema kuwa mkataba huo una kipengele maalumu cha motisha kitakachotolewa endapo timu itafanikiwa kumaliza katika nafasi tano za juu kwenye msimamo wa ligi.
Naye Meneja Masoko wa PigaBet, Arthur Kazora alisema kampuni hiyo imejizatiti kuunga mkono maendeleo ya michezo nchini na kushirikiana na Fountain Gate ni sehemu ya dhamira hiyo.