
Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa mwezi Februari inaelezea visa kadhaa vya ukatili na unyanyasaji wa kingono vinavyowahusisha wanachama wa Misheni ya Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa nchini Haiti (MMAS). Kikosi hiki, ambacho kimsingi kinaundwa na maafisa wa polisi wa Kenya, kilitumwa kuanzia mwaka wa 2024 ili kuwasaidia polisi katika mapambano yao dhidi ya magenge.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa umethibitisha visa vinne vya ukatili na unyanyasaji wa kingono vinavyowahusisha wanachama wa Misheni ya Usaidizi wa Usalama wa Kimataifa nchini Haiti.
Fritznel Pierre ni mjumbe wa kamati ya uongozi ya MMAS, kamati iliyopewa jukumu la kuhakikisha kuheshimiwa kwa haki za binadamu, ambaye anasema matukio yaliyotambuliwa yalitokea katika wilaya ya Petite-Rivière-de-l’Artibonite, lakini anabaini kwamba, idadi halisi ya visa ni kubwa zaidi.
“Hali ya aina hii inazidi kuwa mbaya huko Petite-Rivière-de-l’Artibonite,” amelaani. “Ninazungumzia polisi wa Kenya. Walitumia fursa ya kuona hawachunguzwi na yeyote, na kuanzisha mpango wa ukahaba unaohusisha watoto wadogo. Na kinachosumbua zaidi ni kwamba hata watoto wadogo wenyewe walihusika katika shughuli za aina hii.”
Kumbukumbu za kutisha za MINUSTAH
Kesi hiyo inaamsha kumbukumbu mbaya nchini. Mnamo mwaka 2014, MINUSTAH, Ujumbe wa Utulivu wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, ulirekodi ripoti 13 za unyanyasaji wa kingono na vurugu.
Kati ya mwaak 2004 na 2007, zaidi ya wanajeshi mia moja wa Umoja wa Mataifa kutoka Sri Lanka waliwanyanyasa watoto katika kundi la ukahaba.
Marudio ya tukio ambayo yanatia wasiwasi, hasa kwani wanajeshi wa kwanza wa Chad wa Kikosi cha Kupambana na Magenge wamewasili Haiti. Ujumbe huu pia, umeidhinishwa na Umoja wa Mataifa.