#HABARI: Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaotibiwa saratani katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini (KCMC).

Hatua hiyo imekuja wakati kukiwa na ongezeko la watoto wanaohitaji matibabu hayo ya muda mrefu, ambayo gharama yake inaweza kufikia hadi shilingi milioni 90 kwa mgonjwa mmoja, jambo linalofanya msaada wa wadau kuwa muhimu katika kuunga mkono juhudi za hospitali hiyo.

Licha ya gharama kubwa za matibabu, KCMC imekuwa ikitoa huduma za dawa, upasuaji, na lishe bure kwa watoto wote wanaogundulika na saratani, hali inayosaidia familia nyingi kutoka ndani na nje ya nchi.

Wadau wa afya wamesisitiza kuwa kodi inayokusanywa na TRA ina mchango mkubwa katika kuwezesha upatikanaji wa huduma hizi za kijamii, huku wakitoa mwito kwa jamii kuendelea kusaidia matibabu ya watoto hao ili kuongeza matumaini ya kupona kwao.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *