#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Songwe Ndugu Jabiri Makame ametoa onyo kali kwa watu wanaozua taharuki juu ya taarifa za sehemu za siri za wanaume kutoweka au kupungua ukubwa mara baada ya kushikwa beda na baadhi ya watu kwa kile kinachosadikika ni imani za kishirikina.

Aidha, ametoa onyo kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kuwashambulia watu kwa kuwapiga, kuwajeruhi na kuwasababishia madhara baada ya kutajwa kuhusika na kupoteza sehemu za siri za wanaume.

RC Makame ametoa onyo hilo wakati wa ziara yake aliyoifanya katika Halmashauri ya Tunduma akiwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa kuzungumza na wananchi kuhusu sakata hilo lililoibuka hivi karibuni.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Kisimani, Tunduma Mama Rehema Ngonyani amesema, watu hao wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwani katika Mtaa wake, yupo mwananchi ambaye aliibuka na kudai nyeti zake hazioni baada ya kuguswa na mtu aliyekuwa amekaa naye jirani. Baada ya wanaume wenzake kwenda kumkagua chooni alionekana hana tatizo lolote. Hivyo, aliwaasa vijana kuacha kutumia madawa ambayo yamekuwa yakiwaletea madhara na kuacha kuzua taharuki katika mtaa wake.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *