#HABARI: Kiongozi wa kijeshi wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore, amewataka wananchi wa taifa hilo kusahau kabisa kuhusu masuala ya demokrasia.
Katika mahojiano yaliyotangazwa na televisheni ya taifa ya RTB, Traore alidai kuwa misingi ya demokrasia haikuundwa kwa ajili ya watu wa Burkina Faso, hivyo haina tija kwao kwa sasa.
Hatua hiyo ni muendelezo wa msimamo mkali wa kiongozi huyo aliyenyakua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mnamo Septemba 2022.
Tangu kuingia kwake madarakani, Traore amekuwa akidhibiti sauti za wapinzani kwa nguvu, huku Serikali yake ikivunja Tume ya Uchaguzi mwaka jana na kuzuia shughuli zote za kisiasa nchini humo.
Hali ya kisiasa imezidi kuwa tete baada ya bunge linaloongozwa na wanajeshi kupiga marufuku vyama vyote vya siasa mwezi Februari mwaka huu.
Licha ya Umoja wa Mataifa kutoa mwito wa kurejesha uhuru wa kisiasa na kukomesha ukandamizaji, utawala wa Traore unaonekana kuimarisha kile unachokiita utaratibu mpya wa uongozi usiofuata misingi ya kidemokrasia.
#DWSwahili
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)