
Mashabiki wa timu ya taifa ya soka ya DRC, Leopards, wameipokea timu yao kwa vifijo na nderemo mjini Kinshasa siku yaJumapili hii, Aprili 5. Timu ya taifa ilifuzu wiki iliyopita kwa Kombe la Dunia la 2026, la kwanza tangu mwaka 1974. Wachezaji walirudi katika mji mkuu wa Kongo kwa gwaride mbele ya wafuasi wao kabla ya kuhudhuria sherehe iliyoongozwa na Mkuu wa Nchi katika makao makuu ya Bunge.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Paulina Zidi
Maelfu ya mashabiki wenye shauku walisubiri kwa saa kadhaa Aprili 5 kabla ya hatimaye kuweza kutoa heshima kwa mabingwa wao, ambao walifika jukwaani wakiwa wamejipanga kwenye uwanja wa makao makuu ya Bunge huko Kinshasa Jumapili alasiri.
Walipotoka kwenye basi, wachezaji wa Kongo walilakiwa kwa shangwe kabla ya kuhutubia umati. Kapteni Chancel Mbemba aliiwashukuru mamlaka kwa msaada wake. Kisha, Rais wa Kongo Félix Tshisekedi mwenyewe alizungumza.
Mkuu wa nchi alizungumzia mwisho wa kipindi cha maombolezo cha miaka 52, mwaka wa kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya mwisho kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (wakati huo ikiitwa Zaire) mwaka wa 1974, na zawadi ambazo wachezaji wangepokea baada ya kai yao kubwa ya kihistoria: “Niliahidi kwamba ikiwa wataturudisha kwenye Kombe la Dunia, serikali ya DRC itafanya kila kitu wanachohitaji. Naweza kuwaambia kwamba wachezaji wa Leopards tayari kila mmoja ana nyumba na gari. Pia kutakuwa na zawadi nyingine.”
Mwisho wa kusubiri kwa muda mrefu
Katikati ya sherehe hizo, wakazi wa Kinshasa waliokuwepo walikuwa wakifurahia waziwazi. “Kwa nchi yetu, Kongo, tumekuwa tukisubiri kwa miaka 52. Lakini sasa, hatimaye tunasherehekea!” mmoja wa mashabiki aliyekuja kuishangilia Leopards, amesema. “Ikiwa DRC sasa inazungumziwa katika ulimwengu wa mpira wa miguu, ni shukrani kwa ndugu zetu hawa vijana katika timu ya taifa. Wao ndio bora zaidi; wamefanya yasiyowezekana,” mkazi mwingine aliongeza.
Miongoni mwa wale waliokuwepo kwenye sherehe hio, baadhi walikuwa tayari walicheza Kombe la Dunia. Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa, ambaye alishiriki haswa katika Kombe la Dunia la wachezaji walio naumri wa chini ya Miaka 20 mnamo mwaka 2006 na 2008, alielezea furaha yake: “Tulikuja kusherehekea kufuzu kwao, kwa sababu miaka 52 baada ya Kombe la Dunia lililopita ni muda mrefu. Tuliwafungulia mlango wenzetu, na leo wanacheza Kombe la Dunia. Ni fahari ya nchi yangu!”
Mbele ya umati wa watu wakiimba “Tina trois!” ikimaanisha muhula wa tatu ambao rais wa Kongo anatarajia kuwania ikiwa Katiba itarekebishwa, Félix Tshisekedi alipuuzia swali hilo na kujibu: “Tuko hapa kwa ajili ya Leopards.” Wachezaji hao wanatarajiwa kubaki katika mji mkuu kwa saa chache zaidi kabla ya kurejea Ulaya kwa ndege maalum.