
Nchi ya Ghana, imeungana na Msumbiji pamoja na wadau wengine kususia kongamano la nishati kuhusu bara la Afrika, linalotarajiwa kufanyika kati ya tarehe 12 hadi 14 jijini London nchini Uingereza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kongamano hilo litakuwa muhimu na kuyaleta pamoja mataifa ya Afrika yanayozalisha nishati ya mafuta na gesi barani Afrika.
Hata hivyo, nchi hizo mbili zinasema hazitoshiriki kwa sababu mwandalizi wa kongamano hilo raia wa Uingereza Alexis Bedouin, ameamua kuwatenga wadau muhimu kuelekea kwenye mkutano huo na kutotambua mchango wa watalaam kutoka barani Afrika.
Verner Ayukegba Mwenyekiti wa muungano wa wadau muhimu kwenye sekta ya nishati barani Afrika, ametaka wadau mbalimbali kutohudhuria kongamano hilo kwa sababu, sauti za Waafrika, hazijapewa kipaumbele kuhusu masuala yatakayojadaliwa.
Nao Mawaziri kutoka muungano wa nchi zinazozalisha petroli, wamewakosoa waandamji wa kongamano hilo kwa kuwabagua Waafrika na kutowaajiri kama inavyotakiwa kwenye kampuni za mafuta zilizopo katika nchi zao.