
Serikali ya kijeshi nchini Burkina Faso, imetupilia mbali ripoti ya Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, kuwa zaidi ya raia 1,800 wameuawa katika visa vya uhalifu wa kivita, katika kipindi cha miaka mitatu cha uongozi wa nchi hiyo chini ya Kaptain Ibrahim Traore.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Uongozi wa kijeshi unasema, ripoti hiyo ya Human Rights Watch ni ya uongo, na takwimu zilizotolewa zimetengezwa.
Aidha, serikali ya kijeshi imesema lengo la ripoti hiyo, ni kuvidunisha vikosi vya nchi hiyo ambavyo vimeendelea kufanya kazi kwa weledi, ikiwemo kupigana na makundi ya kijihadi na kigaidi.
Katika hatua nyingine, Burkina Faso imekanusha madai kuwa wanajeshi na washirika wake, wameauwa raia katika matukio 57 kati ya Januari 2023 hadi Agosti 2025, wakiwemo watoto kwa mujibu wa Human Rights Watch.
Katika ripoti yake, Human Rights Watch ilimtaja Traore na Makamanda sita wakuu wa jeshi kuwa huenda walihusika na visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu na wanastahili kuchunguzwa.
Ripoti hiyo pia iliwataja, viongozi watano wa kijihadi kuwa wanapaswa kuchunguzwa kutokana na mauaji ya raia.