Hatua ya serikali ya DRC kuingia kwenye mkataba na Marekani, ili kuwapokea wahamiaji waliofukuzwa katika nchi hiyo, imeendelea kuzua mitazamo mbalimbali.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati wa Lucha na wanasiasa wa upinzani wanapinga mpango huo, ambao serikali ya Kinshasa inasema itagharamiwa kwa asilimia 100 na Marekani.

Vuguvugu la wanaharakati wa Lucha pamoja na wanasiasa wengine huko DRC wamelaani makubaliano yaliyofikiwa na serikali ya Congo ya kuwakaribisha wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani, na kuitaja DRC kuwa jalala la wahamiaji.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotiwa saini Aprili 5 mjini Kinshasa, Kundi la LUCHA linashutumu mpango huo juu ya sera za uhamiaji za Marekani kuelekea nchi yenye kukumbwa na matatizo ya kiusalama eneo la Mashariki, mafuriko na kutokuwepo kwa huduma za kimsingi, na kutaka kufutwa mara moja kwa mkataba huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *