
Rais Trump ametishia kuwa usiku wa leo, Iran itashuhudia hasara na uharibu mkubwa na ustaarabu wote utakuga, iwapo masharti ya kufunguliwa kwa mlango wa bahari wa Hormuz hautafunguliwa kufikia leo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Trump kupitia mitandao wake wa kijamii ya Truth Social, ameonya kuwa iwapo Iran itashindwa kukubaliana na Marekani kwa haraka, basi miaka 47 ya Iran aliyoeleza ya ulafi, ufisadi na kifo yataisha.
Onyo hili linakuja baada ya kiongozi huyo wa Marekani kusema kuwa miundombinu ya nishati na madaraja yatashambuliwa na wanajeshi wa nchi yake.
Hata hivyo, jeshi la kulinda mapinduzi ya Iran limesema litajibu mashambulizi ya Marekani na kuvuka mipaka nje ya eneo la Mashariki ya Kati, katika kile jeshi hilo linasema, mashambulizi yake yatasababisha Marekani na washirika wake kupata changamoto ya miaka mingi ya mafuta na gesi.
Tehran ambayo inaonekana kutotishika na makataa ya Trump imesisitiza kulipiza kisasi hicho iwapo Washington itavuka mstari mwekundu kwa kushambulia miundo mbinu inayotumiwa na raia wa Iran.
Nayo Israeli ambayo imeripoti kuwa Iran imeilenga kwa mashambulizi ya makombora, imewataka raia wa kawaida wa Iran kutotumia usafiri wa treni kwa sababu miundo mbinu ya reli itashambuliwa.