Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimeibua wasiwasi wake kuekekea mabadiliko ya katiba yanayopendekezwa na chama tawala Zanu-PF.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mapendekezo ya ZANU-PF yanalenga kuondoa zoezi la raia kumchagua rais wao, zoezi ambalo limekuwa likifanyika tangu mwaka 1990 na kulipa bunge uwezo wa kufanya hivyo.
Aidha muhula wa Rais unatarajiwa kuongezwa kutoka kipindi cha miaka mitano hadi miaka saba.
Zanu-PF ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka wa 1980 kimetetea mageuzi haya.
Kando na kuongeza muhula wa Rais, muhula wa wabunge pia unatarajiwa kuongezwa kutoka miaka mitandao hadi saba, uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika mwaka wa 2028 ukitarajiwa pia kucheleweshwa hadi mwaka wa 2030.
Mabadiliko hayo sasa yanatarajiwa kumpa Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye muda wake unatarajiwa kumalizika mwaka wa 2028 kusalia ofisini hadi mwaka wa 2030.
Mnangagwa aliingia madarakani mwaka wa 2017 baada ya kuangusha utawala wa Robert Mugabe kupitia mapinduzi ya kijeshi ambapo alishinda uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2018 na 2023.