
Katika mahojiano ya simu na shirika la habari la AFP, Rais wa Marekani Dnald Trump aesema kwamba suala la uranium la Iran “litatatuliwa kikamilifu” kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya wiki mbili yaliyofikiwa na Tehran.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Suala hili litatatuliwa kikamilifu, vinginevyo nisingekubali,” amesema Donald Trump, alipoulizwa kuhusu hatima ya uranium inayorutubishwa na Iran.
Katika mahojiano hayo, pia amesema anaamini China imesaidia kuileta Iran kwenye meza ya mazungumzo ili kuhitimisha makubaliano ya kusitisha mapigano ya wiki mbili. “Hilo ndilo ninalosikia,” amejibu rais wa Marekani, alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Beijing kuhusika katika kuishawishi Tehran, mshirika wake, kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano.
Kwa upande wingine Urusi na China zimepiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Bahrain katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililolenga kulinda usafirishaji wa kibiashara katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Katika kura hiyo, wanachama 11 waliunga mkono azimio hilo, huku China na Urusi wakilipinga, na wanachama wawili wakijizuia.
Kutokana na kura hizo za turufu kutoka kwa wanachama wa kudumu, azimio hilo halikuweza kupitishwa. Waziri wa mambo ya nje wa Bahrain, Abdullatif bin Rashid Al Zayani, amesema azimio hilo limeshindwa kupita kutokana na kura hasi kutoka kwa mwanachama wa kudumu wa Baraza hilo.