
Watu 12 wakiwemo watoto sita wameuawa Kaskazini mwa jimbo la Darfur nchini Sudan, baaada ya kushambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani katika mji wa Kutum.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Viongozi wa kiraia na Madaktari katika eneo hilo, wamethibitisha mauaji hayo, wakati huu jeshi la serikali na wanamgambo wa RSF wakiendelea kupambana tangu mwezi Aprili 2023, kwa kutumia ndege zisizokuwa na rubani.
Miongoni mwa watoto waliofariki ni wasichana watatu wa shule ya Sekondari, ambapo watu wengine 16 wamejeruhiwa, wakiwemo wanawake na watoto.
Jeshi limeshtumiwa kuhusika na shambumizi hili, ambalo limelenga shule ya wasichana ya Al-Um, wakati huu vita vikiendelea.
Mauaji haya yamekuja, baada ya Umoja wa Mataifa wiki iliyopita, katika ripoti yake kueleza kuwa, watu zaidi ya 500 wameuawa kati ya Januari na Machi mwaka huu pekee, katika vita vinavyoendelea, ambavyo vimewaacha watu wengine zaidi ya Milioni 11 wakiwa wametoroka makaazi yao katika mzozo huo unaendelea.