WASHINDI wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu wametangazwa katika hafla ya nne ya utoaji wa tuzo hizo iliyofanyika Aprili 13, 2026 katika Ukumbi wa The Super Dome, jijini Dar es Salaam.
Katika matokeo hayo, Hamisi Kibari ameibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha tamthiliya, huku Bishop Hiluka akishika nafasi ya kwanza katika kipengele cha riwaya. Aidha, Abdalla Ngereza ameshinda katika kipengele cha ushairi, wakati Amina Mohamed aliibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha hadithi za watoto.

Tuzo hizo zinalenga kukuza matumizi ya lugha ya Kiswahili na kuendeleza fasihi nchini kupitia tanzu kuu nne ambazo ni riwaya, ushairi, tamthiliya na hadithi za watoto. SOMA: Serikali Yatenga Bil.4.2 Tuzo ya Uandishi