Dar es Salaam. Sekta ya sanaa na michezo inaendelea kukabiliwa na changamoto za usimamizi wa fedha na kodi. Kwa mujibu wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)  inaonesha kuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ina madai ya fidia ya bima ya ajali Sh239.06 milioni ambayo hayajapokewa kwa miaka 17 sasa. 

Ucheleweshaji huu wa muda mrefu unaashiria udhaifu katika mifumo ya ufuatiliaji wa madeni ndani ya serikali.

Aidha Katika eneo la matumizi, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ilitajwa kupata riba ya Sh446.52 milioni kutokana na kuchelewa kulipa madai ya kimkataba ya makandarasi kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Ukaguzi ulibaini kuwa Wizara ilichelewesha malipo yenye thamani ya Sh7.64 bilioni kwa kipindi cha kati ya siku 23 hadi 101, kinyume na masharti ya mikataba. 

Katika hatua ya kuongeza mapato, serikali imefanya mageuzi ya kodi ambapo sasa kodi ya zuio ya asilimia 5 imeanzishwa kwa ajili ya waundaji wa maudhui ya kidijiti (digital content creators) nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *