Dar es Salaam. Namuona Rich Mavoko kwenye kwato za Juma Nature. Siyo kwamba kabadilika kila kitu, hapana ni yuleyule lakini mapokezi ya ngoma zake siyo kama Rich Mavoko wa WCB.  

Na kitu kimoja wapo ni kwamba mazingira yanaonesha kuwa Rich Mavoko anategemea zaidi kipaji kuliko fujo za kiki nje ya kipaji chake.

Kitu ambacho kilifanya pale WCB aonekane Diamond kwanza kisha Harmonize. Baadaye mashabiki wajichagulie anayefuata kati ya Mavoko na Rayvanny. 

 Siyo kwa uwezo wa kuimba na kutunga mashairi, hapana, kwa maana kwamba alitajwa zaidi Diamond mwenyewe kwenye vinywa vya watu kutokana na aina ya maisha yake, kisha Harmonize.

Hawa jamaa mbali ya muziki wana fujo nyingi za maisha ya mapenzi. Hiki kitu kilimshinda Mavoko akasimamia muziki wake tu. 

 Kwa tabia za Mavoko kutegemea muziki tu, analazimika kuondoka kwenye mizuka ya mashabiki wa WCB na kutengeneza himaya yake ya ‘hapa kazi tu’.

Yote kwa yote mpaka sasa sijamuona Rich Mavoko wa Show Me, aliyemfanya Harmonize atamani ngoma isitoke ili atengeneze ‘verse’ tamu zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *