Mamilioni ya waombolezaji pamoja na viongozi wa kidini, maafisa wa serikali na wageni wa kimataifa wanatarajiwa kuhudhuria kesho katika mazishi rasmi ya Kiongozi Mkuu wa zamani wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei.
Wakati huo huo, mwili wake umeanza kuagwa rasmi leo katika ukumbi wa Grand Mosalla mjini Tehran, ambapo viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho.
Khamenei, ambaye aliongoza Iran kwa takribani miaka 37, anadaiwa kuuawa katika shambulio la anga linalohusishwa na Marekani na Israel, tukio ambalo limezua mshtuko mkubwa na kuibua mabadiliko ya kisiasa nchini humo. Mwandishi wetu, Sauda Hussein, anaripoti kutoka Tehran.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
(Feed generated with FetchRSS)