Mwili wa Ekarist Mushi, mkazi wa Kitongoji cha Vikweme katika Kijiji cha Mikumi mkoani Morogoro, umehifadhiwa kwa siku tatu bila kuzikwa baada ya wananchi kugoma kuuzika wakishinikiza Serikali kuchukua hatua za kudhibiti tembo wanaoingia maeneo yao.

Wananchi hao wamesema tembo wamekuwa wakisababisha vifo vya watu na kuharibu mazao yao, hali ambayo imeendelea kuhatarisha usalama na maisha ya wakazi wa eneo hilo pamoja na kudhoofisha uchumi wa jamii hiyo.

Wakazi hao wanaitaka Serikali kutekeleza maagizo waliyoyatoa, ikiwemo kuhakikisha tembo wanazuiwa kufika maeneo ya makazi ya wananchi. Mwandishi wetu, Theresia Mwanga, anaripoti kutoka Morogoro.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *