Makubaliano ya kusitisha mapigano ya siku kumi kati ya Israel na Lebanon yameanza kutekelezwasiku ya  Alhamisi, Aprili 16, 2026, saa 3:00 usiku, baada ya kutangazwa na Rais wa Marekani Donald Trump. Lakini yalikuwa hayajathibitishwa wakati jeshi la Lebanon liliposhtumu ukiukwaji wa usitishaji mapigano kutoka upande wa Israel kusini mwa nchi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kutangazwa mapema siku hiyo na rais wa Marekani, usitishaji mapigano ulianza kutekelezwa nchini Lebanon saa 3:00 usiku, baada ya siku nyingine ya mapigano makali kati ya jeshi la Israel na Hezbollah, ambayo yalidumu hadi dakika ya mwisho. Lakini saa chache tu baada ya kuanza kutekelezwa usitishaji mapigano, jeshi la Lebanon limeishutumu Israel kwa “ukiukaji kadhaa wa mpango huo.”

Saa chache baada ya makubaliano hayo kuanza kutumika, jeshi la Lebanon limeripoti kwenye mtandao wa kijamii wa X “ukiukaji kadhaa wa makubaliano, vitendo kadhaa vya uchokozi kutoka Israel vikiwa vimerekodiwa, bila kusahau mashambulizi ya hapa na pale yaliyovikumba vijiji kadhaa.”

Jeshi la Lebanon limewataka wale waliohamishwa na mapigano hayo kujizuia kurudi mara moja kusini mwa Lebanon.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *