
Kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) chenye msimamo mkali kutoka mrengo wa kushoto nchini Afrika Kusini, Julius Malema, amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela siku ya Alhamisi, Aprili 16, kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria. Akiwa mtu mwenye utata katika upinzani, anajulikana kwa hotuba zake kali na kupigania ugawaji upya wa mali na kutaifishwa kwa rasilimali. Alifikishwa mbele ya mahakama ya hakimu katika jiji la KuGompo kwa kesi ya miaka minane iliyopita.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès
Nchini Afrika Kusini, kesi hii ni ya mwaka 2018 katik sherehe iliyoandaliwa kwa ajili ya maadhmisho ya kumbukumbu ya miaka mitano ya chama cha EFF. Kiongozi wake, Julius Malema, anatuhumiwa, kwa kisingizio cha sherehe, kufyatua risasi hewani akitumia bunduki ya kivita.
Kama alifutilia mbali ombi la upande wa mashtaka la kifungo cha miaka 15 jela, Jaji Twanet Olivier hata hivyo alitoa adhabu kali kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria. “Baada ya kufikiria kwa makini—na ninataka kukuhakikishia kwamba nimelipa kipaumbele cha juu—nakuhukumu, kwa shtaka la kwanza, kifungo cha miaka mitano jela,” alimwambia kiongozi wa chama cha mrengo wa kushoto cha EFF nchini Afrika Kusini.
Malema analaani uamuzi wa jaji kama “mbaguzi wa rangi.” Julius Malema pia alipokea kifungo cha miaka miwili jela—kitakachohudumiwa kwa pamoja—kwa kumiliki vifaa vya jeshi kinyume cha sheria, pamoja na hukumu zingine ambazo zinaweza kubadilishwa kuwa faini. Alipata idhni kutoka kwa mahakama kukata rufaa dhidi ya hukumu hii, lakini si hukumu iliyomkuta na hatia ya kukiuka sheria za silaha za moto.
Wakati huo huo, bado yuko huru na anaweza kubaki na kiti chake Bungeni. Alipotoka mahakamani, Julius Malema aliwahutubia wafuasi wake, akimtuhumu jaji anayesimamia kesi hiyo kwa kuwa na nia za kisiasa: “Hili halikuwa na uhusiano wowote na sheria. Ni ubaguzi wa rangi alioonyesha. Jaji Olivier ni mbaguzi maarufu wa rangi, na anaujua hilo vizuri sana.”
Upande wa mashtaka, kwa upande wake, ulikaribisha uamuzi huo, ambao ulisema utazuia umiliki wowote wa silaha kinyume cha sheria.