Joe Nam, 55, alifanya kazi katika vyombo vya habari vya serikali kwa miongo mitatu kabla ya kustaafu. Alikuwa ameandika kitabu kinachozungumzia matokeo yanayowezekana ya Rais Yoweri Museveni kujiuzulu baada ya kutawala nchi kwa mkono wa chuma kwa miaka 40.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

rfi”Alipigwa risasi na kuuawa na mtu aliyejificha uso, kulingana na uchunguzi wa awali, saa 7:00 usiku karibu na makazi yake huko Kawanda, katika wilaya ya Wakiso,” Naibu Msemaji wa Polisi Luke Owoyesigyire ameliambia shirika la habari la AFP.

“Mshambuliaji, baada ya kumpiga risasi na kumuua, alikimbia,” ameongeza, akibainisha kuwa uchunguzi “wa kubaini mazingira” ya kifo unaendelea.

Kitabu cha Bw. Nam, “Siku Museveni atakayeondoka: Tafakari, Maswali, Hofu, na Matumaini,” kilitoa ufahamu kuhusu kundi tawal la Rais Museveni, ambalo wanachama wake sasa wanawania kuchukua nafasi yake.

Kiongozi huyo wa Uganda mwenye umri wa miaka 81 alichaguliwa tena kwa muhula wa saba mwezi Januari bada ya uchaguzi ulioshutumiwa na upinzani na kukosolewa na waangalizi wa kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Katika kipindi chote cha kazi yake, Joe Nam alizungumzia masuala ya kisiasa, kiuchumi, na mazingira. Alikosoa rekodi ya serikali kuhusu haki za binadamu na utawala.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *