
Wanajeshi wa Uganda na wenzao wa DRC, wamefanikiwa kuwaokoa raia zaidi ya 200 waliokuwa wametekwa na kundi la kigaidi la ADF, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua ya kuwaokoa raia hao wa DRC ilifanyika, baada ya wanajeshi wa nchi hizo mbili, kutekeleza operesheni ya pamoja katika kmabi ya ADF mwishoni mwa wiki iliyopita.
Jeshi la Uganda limesema, katika operesheni hiyo, magaidi kadhaa wa ADF waliouawa baada ya kulengwa pembezoni mwa Mto Epulu.
Miongoni mwa wale waliokolewa ni wavulana na wasichana kati ya umri wa miaka 14 na 19, huku wakionekana kudhoofika kiafya kwa kukosa chakula na kusumbuliwa na magonjwa kama Malaria.
Baada ya kuokolewa, jeshi la Uganda linasema, linashirikiana na serikali ya DRC ili raia hao warejeshwe kwenye jamii na kuungana na familia zao.
Tangu mwaka 2021, jeshi la Uganda na DRC wamekuwa wakishirikiana katika operesheni ya Shujaa, kupambana na kundi hilo la ADF lililitokea nchini Uganda.