VIWANJANI: “Kwa misimu mitatu mfululizo Feisal ndiye mchezaji bora zaidi kuliko mchezaji yeyote”
Mchambuzi wa soka na mwandishi wa habari mkongwe @nkiniphilip anasema kiungo wa Azam FC, Feisal Salum, ndiye mchezaji anayefanya vizuri zaidi katika ligi ya Tanzania kuliko wachezaji wote wa ndani na hata wageni wanaokuja kucheza nchini.

Nkini anasema Feisal ndiye mchezaji ambaye anamsikiliza zaidi kocha na anafanya yale ambayo anaagizwa kuyafanya uwanjani.

Kwa sasa Fei Toto ndiye mchezaji anayeongoza kwa kuhusika kwenye magoli mengi zaidi akiwa na magoli saba na “assist” saba.

Kwa upande wake mchambuzi @michaelhyera_ anasema kumzungumzia Feisal, utasaidiwa na takwimu zake ambazo amekuwa akiziweka.

(Imeandikwa na @allymufti_tz)

#Viwanjani #FeisalSalum #FeiToto

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *