Nchini Sudan Kusini, serikali imebainisha siku ya Jumanne, Aprili 21, azma yake ya kufanya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba 2026, licha ya hali mbaya nchini humo, ambayo Umoja wa Mataifa unaiona kuwa karibu na vita vya wenyewe kwa wenyewe, huku mamilioni kadhaa ya Wasudan Kusini wakiwa wamekimbia makazi yao au wakimbizi katika nchi zingine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Juba, Florence Miettaux

Uchaguzi huu, ambao tayari uliahirishwa mara nyingi, utakuwa wa kwanza katika historia ya nchi hii changa zaidi duniani, inayoongozwa na Rais Salva Kiir tangu uhuru wake mwaka wa 2011

Sudan Kusini ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka wa 2013, na makubaliano ya amani ya 2018, ambayo yanaeleza uchaguzi, yako katika hali ngumu sana. Lakini Juba inataka kuepuka kwa gharama yoyote kuahirishwa tena kwa uchaguzi huu.

Tume ya taifa ya Uchaguzi ya Sudan Kusini haijapokea ufadhili wowote hadi sasa. Msemaji wa serikali Ateny Wek albainisha siku ya Jumanne kwamba serikali hatimaye itakusanya fedha zinazohitajika kuandaa uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba. “Uchaguzi utafadhiliwa na serikali,” alitangaza, akitaja matumizi ya mapato ya mafuta, huku akikiri “matatizo” yanayoikabili nchi.

Kulingana na afisa huyo, mfululizo wa marekebisho ya makubaliano ya amani ya mwaka 2018 utawasilishwa hivi karibuni kwa Bunge la taifa ili kuruhusu kufanyika kwa uchaguzi. Kwa sababu hatua zilizotolewa katika makubaliano ya amani hazijatekelezwa, uchaguzi hauwezi kufanyika chini ya masharti yaliyotarajiwa na makubaliano. Zaidi ya hayo, Makamu wa rais Riek Machar, mshirika mkuu wa makubaliano ya amani na Salva Kiir, anashikiliwa kizuizini huko Juba, na mapigano yanaendelea kati ya vikosi vyake na jeshi huko Jonglei, kaskazini mashariki mwa nchi.

Chama cha Riek Machar pia kililaani katika taarifa siku ya Jumatatu njia inayotumiwa na kambi ya Salva Kiir kuandaa uchaguzi, njia inayoonekana kuwa “isiyojumuisha wote” na “ikikiuka” makubaliano ya amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *