
Zaidi ya dozi milioni 100 za chanjo zimetolewa kwa watoto milioni 18.3 duniani kote tangu 2023, kama sehemu ya kampeni ya kimataifa ya kupambna na kupungua kwa chanjo ya watoto inayohusishwa na magonjwa ya milipuko, Shirika la Afya Duniani (WHO) na Muungano wa kimataifa wa chanjo GAVI wametangaza Alhamisi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mashirika hayo yalizindua kampeni ya “Massive Catch-Up” wakati wa Wiki ya Chanjo Duniani mwaka wa 2023. Mpango huu, ambao ulilenga watoto wenye umri wa miaka 1 hadi 5 na ulihusisha nchi 36, ulimalizika mwezi Machi mwaka huu.
Takriban watoto milioni 12.3 ambao hawachanjwa hapo awali wamechanjwa dhidi ya magonjwa kama vile diphtheria na polio, mashirika hayo yamesema. Takriban watoto milioni 15 hawakuwa wamechanjwa dhidi ya surua kabla ya kampeni hii. Ingawa data ya mwisho bado inakusanywa, mpango huo wa kimataifa uko katika mstari wa kufikia lengo lake la kuwachanja angalau watoto milioni 21 ambao hawajachanjwa au hawajachanjwa kikamilifu, mashirika hayo yamesema.
Mpango huu unakuja wakati ambapo baadhi ya wafadhili wa jadi, kama vile Marekani, wanapunguza misaada yao, hata kama mamilioni ya watoto wachanga bado hawapati chanjo za kawaida kila mwaka, na kuwaacha katika hatari ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kama vile surua, diphtheria, na polio.
Ephrem Lemango, mkuu wa chanjo katika UNICEF, amesema kwamba kupunguzwa kwa bajeti kubwa hivi karibuni katika afya ya dunia “kumeathiri sana utoaji wa huduma za chanjo” na kunaweza “kufuta maendeleo yaliyopatikana kwa shida.”
Mwaka jana, Waziri wa Afya wa Marekani Robert F. Kennedy Jr., ambaye kwa muda mrefu anashuku chanjo, alikata ufadhili kwa Gavi, shirika linalosaidia kununua chanjo kwa nchi maskini zaidi duniani. Alidai shirika hilo lilikuwa linapuuza wasiwasi wa usalama unaohusiana na chanjo wanazosambaza.
Takriban watoto milioni 14.5 hawakupokea chanjo za msingi kufikia mwaka 2023, huku nchi zilizo katikati ya mzozo wa kimataifa zikishuhudia baadhi ya vikwazo vikali zaidi.