Uwanja wa ndege wa Goma, helikopta ya Umoja wa Mataifa alimo James Swan na ujumbe wake inatua, kisha anakanyaga ardhi ya eneo hili, ikiwa ni mara ya kwanza akiwa Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kufuatia uteuzi wa tarehe 6 mwezi uliopita wa Machi. Wadhifa huu unaambatana pia na kuwa Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini DRC, MONUSCO.

Maamkizi kutoka kwa wenyeji wake ambao ni maafisa wa Umoja wa Mataifa na kisha baada ya itifaki zote kuzingatiwa anasogelea mimbari na kuanza kuzungumza.

Anasema ..“kama mnavyojua, Goma ina nafasi muhimu katika juhudi za sasa za kupunguza mvutano, kulinda raia, na kuunga mkono mchakato wa amani unaoendelea. Uwepo wangu hapa unalenga kwanza kukutana na timu zetu, kusikiliza uchambuzi wao, kubadilishana mawazo na mamlaka zilizojipatia Madaraka, na kuchunguza mazingira halisi ambamo kwayo MONUSCO inaweza kuendelea kutekeleza majukumu yake kulingana na maazimio namba 2773 na 2808 ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.”

James Swan, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Misemo ya Umoja wa Mataifa ya Ulinzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari huko Nord-Kivu, akiwa ameambatana na maafisa wengine na afisa wa jeshi.

Umoja wa Mataifa

James Swan, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) katika ziara yake ya kwanza katika sehemu ya mashariki ya nchi.

Bwana Swan ambaye ni raia wa Marekani amesema ziara yake imekuja wiki moja tu baada ya mazungumzo ya amani ya tarehe 13  hadi 18 mwezi Aprili yaliyofanyika Montreaux, Uswisi kati ya serikali ya DRC na kundi la waasi la AFC-M23 linaloshikilia sehemu ya eneo la Goma, mazungumzo yaliyofanyika chini ya mchakato wa amani wa Doha, unaoratibiwa na Qatar, Marekani, Muungano wa Afrika chini ya uenyeji wa Uswisi.

Hivyo akasema, “tumekaribisha maendeleo yaliyofikiwa kuelekea kutiwa saini kwa itifaki kuhusu ufikishaji wa misaada ya kibinadamu na ulinzi wa kisheria, na tumehimiza pande husika ziendelee kudumisha dhamira yao ili kukamilisha haraka makubaliano haya, kwa lengo la kumaliza mateso yanayokabili raia walionasa kwenyemzozo huu.”

Akageukia masharti yanayopaswa kuzingatiwa ili sitisho la mapigano liweze kudumu, ambapo amesema…masharti haya yanajumuisha kusitishwa kwa matumizi ya droni za mashambulizi, kukomeshwa kwa uingiliaji na uporaji wa ishara za mwelekeo au mienendo (GPS), uhuru kamili wa kusafiri kwa wafanyakazi na vifaa vya MONUSCO, pamoja na matumizi ya viwanja vya ndege na anga. Tunategemea ushirikiano wa pande zote kwenye mzozo ili tusonge mbele haraka katika mwelekeo huu.”

Ziara yake Goma, inafuatia ziara aliyofanya Alhamisi Aprili 23 huko jimboni Ituri, nako mashariki mwa DRC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *