Wakati huo huo nchini Iran, wasiwasi unaongezeka kuhusu uhaba unaokaribia wa vifaa muhimu vya matibabu uliosababishwa na mashambulizi ya mabomu ya Israel na Marekani kabla ya tangazo la kusitishwa kwa mapigano lililotolewa na Rais Donald Trump siku ya Jumatano wiki hii.

“Tangazo la kusitishwa kwa mapigano mapema mwezi huu lilikuwa faraja kubwa. Hata hivyo, hali halisi ilivyo mashinani ni tofauti kabisa,” amesema Cristhian Cortez Cardoza, Naibu Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini katika shirika mshirika wa Umoja wa Mataifa, la Shirikisho la Kimattaifa la Chama cha Msakaba Mwekundu na Mwezui Mwekundu (IFRC).

Mvulana mdogo aitwaye Mahdi amesimama katikati ya magofu ya nyumba ya babu yake iliyoharibiwa huko Beirut, Lebanon, akishika kompyuta. Anaonekana mwenye huzuni, akiwa amezungukwa na mabomoko ya vita, akifikiria kumbukumbu zilizopotea na kutumaini nchi hiyo ijengwe upya.

© UNICEF/Fouad Choufany

Mahdi, mwenye umri wa miaka 10, anatembelea mabaki ya nyumba ya babu yake huko Beirut baada ya kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon.

Akizungumza kutoka Beirut baada ya kurejea kutoka Tehran, Bwana Cardoza amesisitiza kwamba “kusitishwa kwa mapigano haimaanishi kuwa vita vimekwisha.” Athari za wiki kadhaa za “mapigano makali zitaendelea kuhisiwa na jamii ya Iran kwa miezi na hata miaka ijayo,” ameongeza.

Mamamia ya vituo vya afya nchini Iran vimesambaratishwa au kubomolewa, afisa huyo wa IFRC ameeleza, na kuna wasiwasi unaoongezeka kuhusu upatikanaji wa huduma za matibabu na uwezekano wa uhaba wa huduma muhimu kama mashine za kusafisha figo na vifaa vya viungo bandia kutokana na uharibifu wa viwanda.

Kutokana na vita hivyo, kiwanda cha IFRC kinachotoa asilimia 60 ya vichujio vya mashine za kusafisha figo nchini humo kina malighafi ya kutosha kwa miezi mitatu ijayo pekee.

Uharibifu Gaza

Hali bado ni tete huko Gaza, huku zaidi ya vituo 1,800 vya afya vikiwa vimeharibiwa kwa kiasi au kusambaratishwa kabisa, kulingana na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO).

“Inahusisha hospitali kubwa kama Al Shifa mjini Gaza hadi vituo vidogo vya huduma za afya ya msingi, kliniki, maduka ya dawa na maabara,” amesema mwakilishi mpya wa shirika hilo katika Maeneo ya Palestina yanayokaliwa, Dkt. Reinhilde Van de Weerdt.

Akizungumza kutoka Jerusalem, Dkt. Van de Weerdt ameelezea ziara yake ya kwanza Gaza tangu achukue wadhifa huo.

“Nimetumia wiki yangu ya kwanza Gaza mapema mwezi huu. Hakuna kinachoweza kukuandaa kwa kiwango cha uharibifu. Unaweza kusoma ripoti na takwimu, lakini kusimama barabarani katikati ya milima mirefu ya vifusi ni jambo tofauti kabisa.”

media:entermedia_image:8f264327-b9a4-465a-ab7a-e72e969afa44

Mwanamke akimbeba mtoto katika makazi ya hema huko Gaza.

Mahema, vifusi na panya

Katika maeneo mengi ya Gaza, familia nyingi za Wapalestina bado zimekimbia makazi yao.

“Wanaishi kwenye mahema katikati ya vifusi, wakitegemea misaada ya kibinadamu kwa mahitaji yao ya msingi. Na licha ya kusitishwa kwa mapigano, mashambulizi ya anga, makombora na risasi bado vinaendelea,” amesema.

Mbali na hatari hizo, zaidi ya visa 17,000 vya maambukizi yanayohusishwa na panya vimeripotiwa mwaka huu miongoni mwa waliokimbia makazi yao, huku zaidi ya asilimia 80 ya maeneo ya wakimbizi yakiripoti maambukizi ya ngozi kama upele, chawa na kunguni “matokeo yasiyokwepeka wakati watu wanaishi katika mazingira yaliyoharibika,” ameongeza afisa huyo wa WHO.

“Kwa WHO na washirika wa afya, tunahitaji kuelewa vizuri zaidi magonjwa yanayoathiri watu wa Gaza. Tunahitaji vifaa vya maabara na bidhaa zake kuingia Gaza. Kama wengi wenu mnavyojua, vifaa hivi haviingii Gaza, jambo linalotufanya tusione hali halisi.”

Ili kukabiliana na tishio hili la kiafya, “mambo yanapaswa kubadilika,” amesisitiza Dkt. Van de Weerdt. “Wahudumu wa afya wanapaswa kulindwa, dawa na vifaa muhimu lazima viingie Gaza. Vikwazo vya kiutawala na masharti ya upatikanaji vinapaswa kuondolewa.”

media:entermedia_image:67063b1e-acb5-4377-a1cf-aa0f471b100f

Mfanyakazi wa UNMAS anakagua maeneo yaliyoharibiwa na vita Khan Younis, Gaza.

Tishio linalobadilika

Akiunga mkono ujumbe huo, mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma ya Uteguzi wa Mabomu (UNMAS) katika Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Irael ameonya kuhusu hatari ya mabomu ambayo hayajalipuka.

“Tishio hili sasa limejikita ndani ya vifusi,” amesema Julius Dirk Van Der Walt, Mkuu wa UNMAS katika eneo hilo.

“Bado hatujaanza hata kuelewa kikamilifu kiwango cha uchafuzi wa mabomu ambayo hayajalipuka huko Gaza,” ameongeza.

“Tunachojua ni kwamba hili ni tishio linalobadilika familia zitarejea nyumbani, baba anaweza kuingia ndani na kukuta guruneti, na kujaribu kuliondoa ili kulinda watoto wake.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *