Akikabidhiwa mamlaka hayo tangu Aprili 7, James Swan amewasili siku ya Ijumaa, Aprili 24, katika mji mkuu wa Kivu Kaskazini, unaodhibitiwa na AFC/M23, kwa ziara ya siku mbili, ambapo amekutana na viongozi wa kundi hilo lenye silaha.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

James Swan, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, ambaye hivi karibuni aliteuliwa kuongoza Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa unaosimamia amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), akichukua nafasi ya Bintou Keïta, siku ya Ijumaa, Aprili 24, alisafiri hadi Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, ambao umedhibitiwa na waasi wa AFC/M23 tangu mwanzoni mwa mwaka 2025, kukutana na viongozi wa kundi hilo lenye silaha.

Baada ya kushuka kutoka kwenye helikopta yake, James Swan alitoa wito wa utekelezaji wa usitishaji mapigano katika eneo hilo kabla ya kuorodhesha masharti muhimu ya uendeshaji wa Mfumo wa Uthibitishaji wa Pamoja Uliopanuliwa, yaani: kukomesha matumizi ya ndege zisizo na rubani ka mashambulizi, kukomesha kuvuruga mfumo GPS, kuheshimu uhuru wa kutembea kwa wafanyakazi wa MONUSCO, na ufikiaji salama wa anga.

Mkutano na AFC/M23

James Swan kisha alikutana kwa zaidi ya saa tatu na timu ya Corneille Nangaa, mratibu wa Muungano wa kundi hili la waasi. Kufuatia mkutano huo, Corneille Nangaa aliwaambia waandishi wa habari kwamba amemjulisha mkuu mpya wa MONUSCO kuhusu ugumu uliojitokeza katika kutekeleza makubaliano yaliyosainiwa Montreux, nchini Uswisi.

Wakati mapigano yakiendelea na jeshi la Kongo Kaskazini na Kusini mwa mikoa ya Kivu, AFC/M23 pia ilimtaka James Swan kushiriki katika kufungua tena benki huko Goma na kuomba kuanzishwa kwa ndege zitakazodondosha misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa nyanda za juu za Kivu Kusini, ambazo hazifikiki kwa njia ya ardhini. Mwanzoni mwa mwezi huu, shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch lilisisitiza jukumu la pande zote kwenye mzozo huo katika kuzuia utoaji wa misaada na kusafiri kwa raia katika eneo hili.

Ziara ya James Swan huko Goma itaendelea leo Jumamosi, Aprili 25. Ingawa majadiliano zaidi na mamlaka ya AFC/M23 yatafanyika, pia atakutana na maafisa kutoka mfumo wa kikanda ulioundwa ili kufuatilia na kuthibitisha hali ya usalama na makubaliano ya kusitisha mapigano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *