Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) na makundi mengine ya muqawama wa Palestina yamelaani vikali wimbi la sasa la mashambulizi ya Israel katika Ukanda wa Gaza na kuyataja kuwa ni “kuzidisha umwagaji damu na jinai kamili ya kivitaya Wazayuni.”

 Hamas, imesema kupitia taarifa yake ya Jumamosi kwamba mashambulizi ya anga ya Israel, ambayo yameilenga nyumba ya familia moja kaskazini mwa Gaza, gari la polisi huko Khan Younis na kuwauwa shahidi watu zaidi ya kumi, yanadhihirisha  sura halisi ya umwagaji damu mkubwa unaoendelea kufanywa na Tel Aviv  mbele ya macho ya walimwengu.

Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa kuendelea mashambulizi na mauaji dhidi ya Gaza kunakofanywa na serikali ya utawala wa mtenda jinai za kivita Benjamin Netanyahu kunadhihirisha kushindwa wapatanishi, nchi wadhamini na jamii ya kimataifa kuzuia mauaji ya kikatili ya Israel, na kukomesha uhalifu unaoendelea dhidi ya watu wa Palestina.
Hamas imeitaka jamii ya kimataifa na pande zote husika kuchukua hatua za haraka za kuwalinda Wapalestina dhidi ya mauaji ya kila siku jeshi la utawala ghasibu wa Israel, na kuushinikiza utawala huo kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa makubaliano ya usitishaji vita na kuheshimu kanuni za sheria za kimataifa za kibinadamu.
  
  
  
  
  
  
  

 

  
  
  
  
  
  
  
  
  
  
  

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *