Rais Samia Suluhu Hassan, leo Aprili 26, 2026 ametangaza msamaha kwa wafungwa 1,369 ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 62 ya Muungano wa Tanzania.

Kati ya wafungwa hao, 436 wameachiwa huru, huku 933 wakipunguziwa adhabu na kuendelea kutumikia sehemu iliyosalia ya vifungo vyao.

Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobasi Katambi, msamaha huo umezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo wafungwa waliotumikia sehemu ya vifungo vyao, wazee, wagonjwa mahututi, pamoja na wanawake wenye watoto au walioingia gerezani wakiwa wajawazito.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa msamaha huo hauwahusu wafungwa waliopatikana na hatia ya makosa makubwa, yakiwemo ubakaji, unyang’anyi wa kutumia silaha, utekaji, pamoja na uhalifu unaohusisha watoto na rasilimali za taifa.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *