
Waziri wa Vita wa Burkina Faso Célestin Simporé amewasilisha rasimu ya sheria kwa Baraza la Mawaziri siku ya Ijumaa, Aprili 24, kwa ajili ya kuundwa kwa jeshi la akiba. Kulingana na waziri, rasimu hiyo inatoa nafasi ya kuajiri na kutoa mafunzo kwa wanajeshi 100,000 wa akiba ifikapo mwisho wa mwaka 2026, kama sehemu ya mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi. Serikali tayari ilikuwa imeunda kikosi cha watu wanaojitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi (VDP).
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na rasimu ya sheria, akiba hii ya watu 100,000 itaundwa na makundi mawili ya wapiganaji. Kundi la kwanza litaundwa na wafanyakazi wenye uzoefu wa kijeshi, ambao wanaweza kutumwa mara mojakatika uwanja wa vita. La pili litakuwa na raia ambao watafunzwa ili kuimarisha hatua kwa hatua uwezo wa ulinzi.
Kulingana na Célestin Simporé, Waziri wa Vita, “raia wote wenye umri wa kupigana kutetea nchi au kushiriki katika mgogoro wowote wa kibinadamu au mwingine” watafunzwa na wako tayari kuitwa.
Ingawa tayari kuna kikosi cha watu wanaojitolea kwa ajili ya ulinzi wa nchi (VDP), kikosi hiki kinawasilishwa kama “mfumo unaosaidiana, uliopangwa, na wa kudumu” katika muktadha, kulingana na waziri, wa mabadiliko makubwa katika mazingira ya usalama na kisiasa.
Siku ya Jumatano, Aprili 22, shambulio katika sehemu ya mashariki ya kati ya nchi, dhidi ya kambi ya kijeshi ya Bagmoussa katika jimbo la Koulpelogo, liligharimu maisha ya wanajeshi 28 na wanachama wa VDP, kulingana na vyanzo vya usalama.
Na ndani ya mfumo wa Muungano wa Mataifa ya Sahel (AES), Burkina Faso ililaani mashambulizi yaliyoratibiwa yaliyofanywa siku ya Jumamosi na kundi linalodai kuunga kono Uislamu na Waislamu (JNIM, kulingana na kifupi chake kwa Kiarabu) na Kikosi cha Ukombozi cha Azawad (ALF) dhidi ya miji kadhaa mikubwa katika nchi jirani ya Mali.