Iran imechaguliwa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kuwa mmoja wa makamu wenyeviti wa mkutano wa mwaka huu wa kupitia upya Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) utakaoendelea kwa kipindi cha wiki nne.

Kuchaguliwa Iran kumeibua mabishano ya maneno ya hasira kutoka upande wa ujumbe wa Marekani na hivyo kuweka wazi jinsi Washington ilivyotengwa katika majukwaa ya kimataifa.

Mabishano yalitokea katika kikao cha ufunguzi cha mkutano wa kupitia upya Mkataba wa NPT siku ya Jumatatu ambapo mwakilishi wa Marekani alizua ghasia baada ya kuchaguliwa Iran kuwa miongoni mwa makamu wenyeviti 34 wa mkutano huo.

Iran iliteuliwa na Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM), inayowakilisha mataifa 121 yanayoendelea ambayo yanaunga mkono kwa dhati ungamizaji wa silaha za nyuklia na haki ya wazi ya kutumia teknolojia ya nyuklia kwa malengo ya amani.

Mjumbe wa Marekani katika mkutano huo, alionekana kukerwa na alishindwa kuzuia kuchaguliwa Tehran, na kudai kuwa utawala wa Trump “umeshtushwa sana” kwamba nchi ambayo inaituhumu kuudharau mkataba wa NPT imechaguliwa katika nafasi hiyo.

Balozi wa Iran katika ofisi ya Umoja wa Mataifa mjini Vienna Austria, Reza Najafi amekanusha vikali tuhuma za Marekani na kuzitaja kuwa hazina msingi na kwamba zinatokana na matashi ya kisiasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *