
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, makataa ya yaliyokubaliwa kati ya waasi wa M23/AFC na serikali ya Kinshasa, kuachiliwa huru kwa wafungwa kutoka pande zote, yamepita bila ya kutekelezwa.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Aprili tarehe 28, ilikuwa ndio siku ya mwisho kwa waasi na serikali kuwaachilia wafungwa hao kwa mujibu wa makubaliano yaliyoafikiwa na pande zote wiki kadhaa zilizopita wakati wa mazungumzo ya amani nchini Uswizi.
Hata hivyo, hakuna haya mfungwa mmoja aliyeachiliwa. Kwa upande wa waasi wa M23/AFC inawashikilia wafungwa 311 huku serikali nayo ikiendelea kuwashikiliwa wafungwa 166 washirika wa waasi hao.
Kwa mujibu wa makubaliano ya Uswizi, kila upande unatakiwa kuonesha utayari wa kuwakabidhi wafungwa hao kwa shirika litakalofanikisha zoezi hilo.
Ripoti za ndani zinasema, tayari waasi wa AFC/M23 iliwasilisha orodha ya wafungwa inayotaka waachiwe, lakini upande wa serikali haujafanya hivyo, wakati huu kukiripotiwa mgawanyiko ndani ya serikali kuhusu mpango huo.
Kutokana na hali hiyo na serikali ya Kinshasa kutoonekana kuwa tayari kuwaachia huru baadhi ya wafungwa, ripoti za kidiplomasia zinasema, orodha mpya huenda ikajadiliwa kabla ya makubaliano hayo kutekelezwa.