
Watu zaidi ya Milioni nane nchini Sudan Kusini, wapo kwenye hatari kubwa na kukabiliwa na njaa kali kufuatia kuendelea kwa vita vinavyosababisha maelfu ya watu kuyakimbia makaazi yao.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti ya Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa hali ya kibinadamu ni mbaya na asilimia 56 ya watu kwenye taifa hilo watakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula katika miezi kadhaa inayokuja.
Tayari watoto wenye kati ya umri wa miezi sita na miaka mitano wanakabiliwa na tatizo la utapiamlo kwa kukosa lishe bora, ambapo idadi hiyo imeongezeka kwa 100,000 na kufikia watoto Milioni 2.2.
Wakati huu watoto 700,000 wakihofiwa kuwa huenda wakapoteza masiha kwa sababu ya njaa, mashirika ya Umoja wa Mataifa yakiongoza na lile la mpango wa chakula WFP na linaloshughulikia watoto UNICEF, yanatoa wito kwa jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatau za haraka ili kuzuia janga la kibinadamu.
Kliniki nyingi zinazotoa huduma kwa watoto, zimefungwa na zingine kuharibiwa katika maeneo mengi nchini Sudan Kusini kwa sababu ya vita.