
Waziri wa Mawasiliano na Vyombo vya Habari wa DRC, Patrick Muyaya, ameuwasihi umma kuwajibika na kuwa watulivu kuhusu uwepo wa wahamiaji nchini hmo. Katika mahojiano na Redio na Televisheni ya serikali, RTNC, msemaji wa serikali alionya dhidi ya kuenea kwa taarifa potofu na matamshi ya chuki kwenye mitandao ya kijamii.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na Waziri huyo, wageni ambao uwepo wao unasababisha wasiwasi wanaishi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kisheria kabisa. Patrick Muyaya alifafanua kwamba kukaa kwao ni kwa muda mfupi na kunafanywa chini ya usimamizi mkali wa mamlaka husika.
Mchakato wa kurudi kwa wahamiaji
Serikali inauhakikishia umma kwamba jambo hili linafuatiliwa kwa ukaribu. Ukaguzi wa mara kwa mara unafanywa ili kuhakikisha kufuata kanuni za uhamiaji.
“Majadiliano yanaendelea na nchi zao za asili ili kuandaa kurejea kwao kwa wakati uliopangwa,” alisema Waziri wa Mawasiliano.
Kupambana na taarifa potofu
Kutokana na kuenea kwa baadhi ya jumbe za kutisha, serikali inatoa wito wa kuwa macho. Wakati akisisitiza tena kujitolea kwake kwa uhuru wa kujieleza, Patrick Muyaya anawasihi watumiaji wa intaneti kutoshiriki ujumbe unaoweza kusababisha hali ya hofu au chuki dhidi ya wageni katika jamii.