Aliyekuwa mjumbe wa bodi ya wadhamini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Anna  Komu amefariki dunia saa tatu usiku wa jana Jumanne Aprili, 2026 Zanzibar.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), Amani Golugwa ameithibitishia Mwananchi leo Jumatano Aprili 29, 2026 juu ya kifo mwanachama wake, aliyewahi kuwa Mbunge wa Viti Maalumu na mgombea mwenza wa urais 2005.

Maulida alikuwa ni mmoja ya waliofungua kesi dhidi ya bodi ya wadhamini ya Chadema, wakidai chama hicho kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasilimali fedha. 

Kesi hiyo inaendelea Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam. 

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, Anna MaulidaKomu aliteuliwa na Chadema kuwa mgombea mwenza wa urais baada ya Jumbe Rajab Jumbe kufariki dunia zikiwa zimesalia nne kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu Oktoba 26, 2005.

Uchaguzi huo uliahirishwa hadi Desemba 18, 2005 na Chadema kumteua Anna. Wakati huo, mgombea urais wa Chadema alikuwa Freeman Mbowe.

Endeleea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *