Marekani imebainisha uwezekano wa kuzingirwa kwa muda mrefu kwa bandari za Iran siku ya Jumatano, Aprili 29, jambo ambalo litazidisha shinikizo kwa uchumi wa dunia, na athari ya haraka kwa bei ya mafuta, ambayo imepanda hadi kiwango cha juu zaidi katika miaka minne.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Jaribio lolote la kuweka kizuizi cha baharini ni kinyume na sheria ya kimataifa (…) na litashindwa,” Massoud Pezeshkian amesema katika taarifa, baada ya afisa mkuu wa Ikulu ya White House kupendekeza kuongeza kizuizi hicho “kwa miezi kadhaa.”

Ingawa taarifa hizi zilichangia kuongezeka kwa bei ya mafuta, rais wa Iran amesema kwamba hatua hizo za kuzingirwa “sio tu kwamba zinashindwa kuboresha usalama wa kikanda, lakini pia zinaunda chanzo cha mvutano na kuvuruga utulivu wa muda mrefu wa Ghuba.”

Wakati huo huo Rais wa Marekani Donald Trump amekuwa akijadiliana na makampuni ya mafuta jinsi ya kupunguza athari za kuzingirwa kwa bandari za Iran kwa miezi kadhaa na Marekani, afisa wa Ikulu ya White House alisema siku ya Jumatano, Aprili 29. Tehran, kwa upande wake, ilionya kuhusu “hatua za kijeshi ambazo hazijawahi kutokea” ikiwa Marekani itaendelea kuzuia meli zinazohusiana na Iran.

Kutokana na pendekezo la Washington la kuzuiwa kwa muda mrefu kwa Mlango-Bahari wa Hormuz, bei ya mafuta imepanda tena eo Alhamisi, huku mafuta ghafi ya Brent, kiwango cha kimataifa, ikipanda kwa 5% hadi karibu dola 125 kwa pipa. Tangu siku ya Jumatano, bei zimefikia viwango ambavyo havijaonekana tangu katikati ya mwaka wa 2022, wakati uvamizi wa Urusi nchini Ukraine uliposababisha ongezeko la bei.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *