Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limeshambulia na kuharibu kambi na maeneo kadhaa muhimu ya kijeshi ya Marekani katika nchi za Jordan, Bahrain, Kuwait na Oman katika operesheni ya kulipiza kisasi ya awamu tano dhidi ya uchokozi wa Marekani, ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya nchi hiyo katika maeneo ya pwani ya Iran.

IRGC leo imetoa taarifa mfululizo ikieleza kwamba oparesheni hizo ni majibu ya awali dhidi ya hujuma za Marekani. Jeshi la Iran pia limethibitisha kwamba mtandao wake jumuishi wa ulinzi wa anga umezuia na kuharibu ndege isiyo na rubani ya adui (droni) katika mji wa bandari wa kusini.

Ofisi ya Uhusiano wa Umma ya Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetangaza kuwa: Droni ya kivita aina ya “Lucas” ya adui mchokozi imefuatiliwa na kushughulikiwa kwa mafanikio na mfumo wa makombora ya ardhini – angani unaoendeshwa na Kikosi cha Ulinzi wa Anga huko Bandar Abbas.

Taarifa ya kwanza ya IRGC ilitolewa usiku wa kuamkia leo kufuatia tukio lililohusisha meli mbili zilizokiuka sheria ambazo zilikuwa zimehatarisha usafiri wa baharini katika Lango-Bahari la Hormuz. Taarifa hiyo imesema, jeshi la Marekani kwa mara nyingine tena limedhihirisha asili yake ya ukatili kwa kushambulia kambi za pwani za Iran.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limesema: “Wapiganaji watukufu wa Kiislamu wamechoma vituo kadhaa vikubwa vya makombora na matangi ya kuhifadhia mafuta katika Kituo cha Anga cha Prince Hassan nchini Jordan kwa kukipiga kwa makombora na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *