Mataifa 53 ya Afrika, isipokuwa Eswatini, kuanzia leo Mei tarehe 1, itaanza kusafirisha na kuuza bidhaa zake nchini China bila kutozwa ushuru.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii kati ya Beijing na bara la Afrika, inatarajiwa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara katika mkataba ambao unatarijiwa kuendelea hadi tarehe 30 mwezi Aprili mwaka 2028.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya uchumi na biashara wanaona kuwa China ndio itakayofaidika zaidi, ikilinganishwa na Afrika ambayo baadhi ya mataifa hayana bidhaa za kutosha kuuza kwenye soko la nchi hiyo.

Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaona hatua ya China kama njia moja ya kujaribu kuongeza ushawishi wake barani Afrika kwa lengo la kuipiku Marekani.
Wachambuzi wa masuala ya uchumi wanaona hatua ya China kama njia moja ya kujaribu kuongeza ushawishi wake barani Afrika kwa lengo la kuipiku Marekani. © Evelyn Hockstein / Reuters

Hatua hii inamaanisha pia kuwa bara la Afrika limefungua mlango  kwa China kuchukua malighafi zake kama mafuta na madini, na kuziongezea thamani kabla ya kuziuza tena.

Aidha, ni hatua inayoonekana kuwa ya kisiasa na ushindani dhidi ya Marekani kwenye ushirikiano wake wa kibiashara na mataifa ya Afrika, inakuja wakati huu Washington ikiongeza ushuru kwa bidhaa zinazoingia nchini mwake huku China ikifuta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *