Miaka nane baada ya taifa la kenya kupiga marufuku vifungashio vya plastiki, tatizo hili bado ni kero hasa katika mpaka wa Busia, kati ya Kenya na Uganda.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kaunti ya Busia ni mojawapo ya Miji inayokabiliwa pakubwa na changamoto hii hasa ukizingatia kuwa hili upo kwenye mpaka wa  kenya na uganda, ambapo vifungashio hivi vinakubalika kutumika.

Ongezeko hili limeathiri kwa kiwango kikubwa hatua za kutekeleza sheria zilizowekwa za kuviondoa nchini kenya.

Kesi za matumizi ya mifuko ya plastiki zimewasilishwa katika mahakama za Busia, washukiwa wakihukumiwa na vifungio hivi kuchomwa ili visiweze kuingia sokoni.

Cliff bonchari ni mkurugenzi mkuu wa idara ya mazingira kaunti ya Busia.

“Ingawa sheria za matumizi ya mifuko ya plastiki kwa bidhaa kama mikate na sukari yalihalalishwa kisheria, ni lazima anayetumia aweze kuwa na leseni. Tunakuwa na changamoto kubwa kwa wale wanaoingiza vifungio hivi nchini ila sheria itazidi kichukuwa mkondo wake ” alisema Cliff bonchari ni mkurugenzi mkuu wa idara ya mazingira kaunti ya Busia.

Hakimu  katika idara ya mahamaka mjini Busia anaeleza uamuzi uliopelekea kuchomwa kwa makaratasi hayo.

“Kila mkenya anafaa kufahamu kuwa chochote ambacho hakiruhusiwi nchini kisheria, hata kama kinaruhusiwa kwingine, ni vyema azingatie sheria ya Kenya alisema Hakimu  katika idara ya mahamaka mjini Busia.

Agnes achieng  mfanyibiashara wa samaki  na Novet Samanya mkaazi wa busia wanaelezea sababu za kutumia vifungio hivyo.

“Makaratasi haya ni mazuri kwa kufungia wateja haswa watoto na pia yanazuia bidhaa kuharibika wakati wa mvua. Bei yake pia ni nafuu ikilinganishwa na  mifuko iliyoidhinishwa kenya”.

Serikali inazidi kuweka mikakati ya kutekeleza sheria hiyo iliyoidhinishwa mwaka 2017. 

Petronila Ogalo, Busia RFI kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *