KOCHA wa Yanga, Pedro Goncalves ameanza kuonyesha mbinu zake kuelekea dabi dhidi ya Simba baada ya kuonekana akiwaweka kando baadhi ya mastaa wa timu hiyo na kufanya nao vikao wakati wakiendelea kujifua katika mazoezi huko Zanzibar.

Yanga Aprili 29, 2026 ilipoteza mchezo wa fainali wa Kombe la Muungano kwa kulala bao 1-0 dhidi Simba katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar na sasa inatarajiwa kujiuliza kwenye Dabi ya Ligi Kuu Mei 3, 2026 kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.

Katika mazoezi ya kujinoa na dabi, Pedro alionekana akianza kwa kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua kabla ya kuendelea na straika Prince Dube, kisha Allan Okello na kuhitimisha na Duke Abuya ambaye kwenye mchezo uliopita alianzia benchi.

MASTA 02

Mmoja kati ya viongozi wa klabu hiyo aliliambia Mwanaspoti kuwa, kocha huyo alionekana akitumia muda mrefu kuzungumza na nyota hao, mara nyingi akisisitiza maelekezo kwa kutumia ishara za mikono, akionyesha wazi kuwa anataka kila mchezaji kuelewa majukumu yake kabla ya mchezo huo mkubwa.

“Baadhi ya vikao vilifanyika kabla ya mazoezi kuanza, huku vingine vikiendelea hata baada ya mazoezi kumalizika, ishara kuwa benchi la ufundi linapanga kwa umakini mkubwa mbinu za kuivaa Simba, kocha alianza kufanya mazungumzo.

MASTA 01

“Hatua hiyo inaonyesha namna kocha alivyojipanga kuhakikisha timu inapata matokeo chanya kwenye dabi hiyo, hasa baada ya presha ya kupoteza Kombe la Muungano, jambo lililowaacha na deni kwa mashabiki wao.” Mbali na maandalizi hayo, rekodi zinaonyesha Yanga imekuwa na mwenendo mzuri katika mechi za hivi karibuni za dabi, ikiwa imefanikiwa kushinda michezo muhimu dhidi ya Simba, jambo linaloweza kuwapa morali kuelekea pambano lijalo.

MASTA 03

Yanga inaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo 19 ikiwa na pointi 47 ambazo ni tano nyuma ya Simba inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *