Nigeria imetangaza mpango wa kuwarudisha nyumbani raia wake, kutoka nchini Afrika Kusini, wakati huu kukiwa na hofu kubwa ya kuendelea kwa wimbi la kuwashambulia wageni hasa Waafrika katika nchi hiyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Nigeria, Bianca Odumegwu-Ojukwu amesema raia wa nchi yake wapatao 130 tayari wameomba msaada wa serikali ili waondoke nchni Afrika Kusini kwa kushambuliwa na biashara zao kuharibiwa.

Aidha, Waziri huyo ameongeza kuwa kwa sababu ya kuendelea kwa hofu ya wageni hasa waafrika kushambuliwa nchini Afrika Kusini, idadi ya raia wa Nigeria wanaotaka kuondoka, huenda ikaongezeka.

Tangazo hili linakuja, huku rais Bola Tinubu, akilaani matukio ya kuendelea kushambuliwa kwa raia wa nchi yake nchini Afrika Kusini, akisema vitendo hivyo havikubaliki.

Balozi wa Nigeria jijini Pretoria, alikutana na mwenzake wa Afrika Kusini siku ya Jumatatu kuonesha masikitiko yake, wakati huu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, ukionekana kuyumba.

Nigeria inasema raia wake wawili wameuawa nchini Afrika Kusini, katika siku za hivi karibuni na inataka haki kutendeka, huku raia wa nchi hiyo wakiwalaumu wageni hasa wale kutoka nchini Nigeria kwa kuendeleza biashara ya dawa za kulevya na kushiriki kwenye visa vya utovu wa usalama katika nchi yao.

Hii sio mara ya kwanza kwa Afrika Kusini, kukabiliwa na changamoto hii ambapo takwimu zinaonesha kuwa asilimia tano ya watu wanaoishi nchi hiyo, sawa na watu Milioni tatu ni wageni wanaoishi nchini humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *