Waasi wa ADF Mashariki ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo wametekeleza uhalifu mkubwa dhidi ya bindamu, hii ni kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty International.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

ADF wameripotiwa kutekeleza mauaji ya watu, utekaji nyara, kuwatoa wanawake mimba kwa lazima, kulazimisha ndoa za mapema, kubaka wanawake na wasichana pamoja na kuwadhulumu watoto.

Waasi hao wanaoshirikiana na makundi ya kigaidi ya ISIS/ISIL, kwa miaka kadhaa wamekuwa wakitekeleza mashambulio dhidi ya raia mashariki ya Congo haswa katika miji jirani na Uganda.

Mashambulio ya ADF yamewalazimu maelfu ya raia kutoroka makazi yao katika baadhi ya Miji ya Mashariki ya Congo, wengine wakishindwa kupata matibabu, elimu na hata chakula kutokana na shida ya usalama.

Aidha uasi wa M23 umeripotiwa kulipa nguvu kundi hilo kuendelea na harakati zake nchini DRC,  hali ikiripotiwa kuwa mbaya zaidi kutokana na kwamba nguvu kubwa ya Kinshasa na jamii ya kimataifa imeelekezwa kwa M23/AFC.

Amnesty iliwahoji watu 71 wakiwemo waliojeruhiwa katika mashambulio ya ADF, maofisa wa usalama na wafanyikazi wa mashirika ya misaada huko Kivu kaskazini ambapo uasi unazidi kuripotiwa.

Katika mojawapo ya mashambulio mabaya zaidi kutekelezwa na ADF, lilikuwa lile la Septemba mwaka 2025 katika kijiji cha Ntoyo ambapo waliuwa watu zaidi ya 60.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *