Baada ya mwezi mmoja akiwa kifungoni mikononi mwa Boko Haram, daktari wa watoto kutoka Chad ameachiliwa huru Jumatatu jioni. Taarifa hii, iliyoripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya Tchadinfos, ilithibitishwa kwa RFI na chanzo rasmi cha Chad leo Jumanne asubuhi.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Chanzo hicho kimekataa kutoa maelezo ya kuachiliwa kwake. Mamlaka ya Chad innamrudisha kutoka Niger, ambapo kwa sasa yuko katika mji wa mpakani karibu na eneo alilotekwa.

Daktari huyo wa watoto alichukuliwa mateka pamoja na watu wengine sita wakati gari lao liliposhambuliwa katika eneo la jangwani.

Abiria mmoja aliuawa na wanajihadi. Wafungwa wengine watano waliachiliwa huru nchini Niger katika wiki zilizofuata baada ya kulipa fidia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *