Shirikisho la Soka la Palestina limechapisha ripoti kuhusu mauaji ya wachezaji wa mpira wa miguu na uharibifu wa miundombinu ya soka uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Shirikisho la Soka la Palestina leo (Jumanne) limetoa bango linaloonyesha jinsi utawala wa Israel unavyopiga mabomu katikati ya viwanja vya mpira chini ya kivuli na kimya cha Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), ikiwa ni jibu la haraka na madhubuti kwa hatua ya kuaibisha ya rais wa FIFA katika Mkutano wa 76 wa FIFA uliofanyika wiki iliyopita nchini Canada.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni kutoka Shirikisho la Soka la Palestina, utawala ghasibu wa Israel umewaua wachezaji 566 wa mpira wa miguu wa Kipalestina tangu Oktoba 2023.

Licha ya uhalifu huo wote wa Israel dhidi ya jamii ya mpira wa miguu ya Palestina, Rais wa FIFA, Gianni Infantino wiki iliyopita alijaribu kuweka mkono wa Jibril Rajoub, Rais wa Shirikisho la Soka la Palestina, kwenye mkononi mwa makamu wa rais wa Shirikisho la Soka la Israel, jambo ambalo lilipingwa vikali na rais wa Shirikisho la Palestina, na kumfanya Infantino kushikwa na tahayuni kadamnasi.

Shirikisho la Soka la Palestina linaripoti kwamba Israel sio tu inawaua wachezaji wake wa mpira wa miguu katika ukimya wa FIFA na bila kuchukuliwa hatua yoyote, lakini pia imebomoa au kuharibu vituo 152 vya mpira wa miguu katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi.

Ripoti ya Shirikisho la Soka la Palestina inasema, Israel imewajeruhi na kuwatia ulemavu wachezaji wa mpira wa miguu 44 na kuwafunga jela wengine 24 tangu Oktoba 2023.

Katika mkutano wa wiki iliyopita wa FIFA uliofanyika huko Canada, Suzanne Shalabi, naibu mkuu wa Shirikisho la Soka la Palestina, aliiambia Reuters kwamba Rajoub alisema: “Siwezi kupeana mikono na mtu ambaye Waisraeli wamemleta ili kutakasa uhalifu wao wa kifashisti na mauaji ya kimbari.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *