Televisheni ya CNN imeripoti kuwa, ikiwa imepita zaidi ya miaka minne baada ya ndege ya abiria ya Boeing 737-800 kuanguka mlimani kusini mwa China na kuua watu wote 132 waliokuwa ndani yake, data iliyotolewa hivi karibuni “imeashiria kwambs upo uwezekano mtu aliyekuwa katika chumba cha marubani alizima usambazaji wa mafuta katika injini kwa makusudi.

Maafa hayo ni miongoni mwa ajali mbaya zaidi za anga kuwahi kutokea nchini China katika miaka ya hivi karibuni, lakini Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) bado haijabaini chanzo cha ajali hiyo mbaya ya ndege ya China Eastern Airlines MU5735 iliyotokea mwezi Machi 2022 katika mkoa wa Guangxi.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Usalama wa Uchukuzi ya Marekani (NTSB) imeonyesha kuwa swichi za mafuta za injini zote mbili zilizimwa kwa wakati mmoja kabla ya ndege hiyo ya Boeing 737-800 kuanguka.

NTSB imeeleza kuwa “Ilibainika kuwa wakati ndege hiyo ya China iliporuka umbali wa futi 29,000 (mita 8,840), swichi za mafuta kwenye injini zake zote mbili zilikumbwa na hitilafu. Kasi ya injini ilipungua wakati wa kubadili mafuta.

Mchambuzi wa masuala ya usalama wa anga wa CNN anasema: Swichi za mafuta kwenye ndege za kibiashara ni vidhibiti vya mwongozo vinavyodhibiti mtiririko wa mafuta kwenye injini.

David Soucie anasema: Katika ndege hiyo ya Boeing 737-800 data hii inaonyesha wazi kuwa swichi za mafuta zilibadilishwa na kuwekwa katika sehemu ya kuzima (Off) kabla ya kutokea ajali. 

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya China (CAAC) imekanusha madai kwamba ajali hiyo ya ndege ilipangwa kwa makusudi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *