
Shambulio linalohusishwa na Boko Haram, ambalo lilitokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne katika kambi ya kijeshi ya Barka Tolorom magharibi mwa Chad, upande wa Chad wa Ziwa Chad, limegharimi maisha ya watu zaidi ya 20 na wengine kadhaa kujeruhiwa, kulingana na duru za kuaminika zilizozungumza na RFI siku ya Jumanne.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Taarifa kutoka kwa makao makuu ya Jeshi iliripoti “watu 23 waliouawa na 26 waliojeruhiwa” miongoni mwa Vikosi vya Ulinzi na Usalama. “Idadi kubwa ya washambuliaji kutoka kundi hili la Boko Haramu iliuawa na vifaa vya kijeshi vilikamatwa, na operesheni ya utafutaji inaendelea,” taarifa hiyo ilisema. Kijiji jirani pia kilichomwa moto na mali kuporwa. Hakuna taarifa kuhusu idadi ya vifo vya raia. Shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali katika eneo hilo zimesitishwa kwa sasa.
Jeshi la Chad lililengwa tena na shambulio baya juzi usiku katika eneo la Ziwa Chad. Makao makuu ya jeshi yameripoti shambulio la wanajihadi wa Boko Haram katika kambi ya jeshi, na kutoa idadi ya awali ya watu 23 waliouawa na 26 waliojeruhiwa.
Kulingana na taarifa kutoka makao makuu ya jeshi, yapata saa nne usiku Jumatatu, watu wenye silaha walivamia kituo cha kijeshi kilichopo kwenye Kisiwa cha Barka Tolorom, katika sehemu ya Chad ya Ziwa Chad.
Jeshi linawatambua washambuliaji hao kama wapiganaji wa Boko Haram, bila kutaja ni kundi gani, na linadai kuwa limeangamiza idadi kubwa ya washambuliaji hao, bila kutoa idadi kamili, na kukamata vifaa vya kijeshi na kuendelea na shughuli zake za utafutaji.
Pongezi kutoka kwa Mkuu wa Nchi
Katika ukurasa wake wa Facebook, Rais Mahamat Idriss Déby alikaribisha ujasiri wa wanajeshi, “mashujaa” walioanguka vitani, na kutoa rambirambi zake kwa familia zao.
Jeshi la Chad hulengwa mara kwa mara na makundi ya wanajihadi katika eneo la Ziwa Chad. Mnamo mwezi Machi 2020, shambulio katika kambi ya Bohomaliligharimu maisha ya karibu wanajeshi 100 wa Chad. Mnamo mwezi Oktoba 2024, shambulio lingine baya lilisababisha vifo vya watu zaidi ya arobaini.