
Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza siku ya Jumanne jioni, Mei 5, kwamba “maendeleo makubwa” yamefanywa kuelekea makubaliano ya “mwisho” kati ya Marekani na Iran, akibainisha kwamba kwa hivyo ameamua kusitisha Operesheni “Project Freedom”, iliyozinduliwa siku moja kabla, ili kuhakikisha usafiri wa meli za kibiashara kupitia Mlango wa Hormuz.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Rais Donald Trump alitangaza siku ya Jumanne, Mei 5, kwenye mtandao wake wa Truth Social, kusitishwa kwa “kipindi kifupi” cha misheni ya kijeshi ya Marekani ya kusindikiza meli zilizokwama katika Ghuba ili kuhakikisha zinapita salama kupitia Mlango wa Hormuz. Rais wa Marekani anakusudia kutumia hili kubaini kama makubaliano yanaweza kusainiwa na Tehran.
Mapema, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisema kwamba Marekani imefikia malengo ya kampeni yake ya kijeshi nchini Iran, ingawa Washington haikuwa imechukua akiba ya uranium iliyorutubishwa ya Tehran. Awamu ya mashambulizi ya mzozo na Iran “imekwisha,” alitangaza.
Kikosi cha Walinzi wa mapinduzi wa Iran waliahidi siku ya Jumanne, Mei 5, “jibu thabiti” kwa meli zinazojaribu kuvuka Mlango-Bahari wa Hormuz kwa njia yoyote ile isipokuwa ile waliyotangaza.