Nchi ya Cape Verde na Hispania, zimekataa kupokea meli ya kitalii, MV Hondius kutoka Uholanzi, iliyo na watu 140, wakiwemo abiria 80 kutoka mataifa 15, ambao baadhi yao wameambukiwa virusi hatari vya  hantavirus.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hispania imebadilisha maamuzi yake, licha ya hapo awali, kueleza kuwa ingepokea meli hiyo, ambayo abiria wake wameambukizwa virusi hivyo hatari vinbavyoambukizwa kwa haraka baina ya binadamu.

Kwa sasa meli hiyo, imekwama katika pwani ya kisiwa cha Cape Verde, huku kiongozi wa kisiwa cha Canary, Fernando Clavijo, akisema meli hiyo haiwezi kukubaliwa kutia nanga kwa sababu mamlaka haina taarifa za kutosha kuhusu mlipuko wa ugonjwa huo.

Abiria wanane wameambukizwa, akiwemo raia wa Uingereza, anayeendelea kupewa matibabu nchini Afrika Kusini huku maafisa wa afya wakisema waliombukizwa wanaendelea na matibabu.

Shirika la afya duniani WHO tayari limethibitisha kuwa, abiria watatu wamepoteza maisha kutokana na maambukizi ya virusi hivyo.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema haamini iwapo virusi hivi ni kama vile vya Uviko 19 vilivyotikisa dunia miaka kadhaa iliyopita.

Hantavirus ni aina ya virusi vinavyopatikana kwenye wanyama kama panya, na mara nyingi binadamu huambukizwa virusi hivyo kwa kupumua hewa inayotokana na kinyesi cha panya kilichokauka au kugusa mkojo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *