Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa, Vasily Nebenzya, amepinga vikali azimio lililopendekezwa na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Baraza la Usalama. Amelitaja azimio hilo kuwa ni jaribio jingine lenye mtazamo wa uhasama, linalolenga kuizingira Iran huku likipuuza mizizi halisi ya mzozo wa sasa wa Ukanda wa Asia ya Magharibi.

Nebenzya alitoa kauli hizo Alhamisi jioni wakati wa majadiliano kuhusu usalama wa baharini katika Ghuba ya Uajemi, eneo ambalo Marekani na washirika wake wamekuwa wakisukuma mswada wa maazimio ambayo wakosoaji wanasema yanailenga Iran kwa njia isiyo ya haki, hususan kuhusu hatua zake za kujilinda katika Mlango-Bahari wa Hormuz.Moscow imesisitiza mara kadhaa kwamba haitaiunga mkono hati yoyote inayoioonyesha Iran kama yenye makosa bila kushughulikia sababu za msingi za mivutano — ikiwemo uchokozi wa Marekani na ‘Israel’ dhidi ya Iran ambao ni sababu ya msingi ya ukosefu wa utulivu hivi sasa katika eneo zima.Mwanadiplomasia huyo wa Russia amesisitiza kuwa usalama wa kweli wa meli zinazopita katika Ghuba ya Uajemi hauwezi kupatikana kwa lawama za upande mmoja au hatua za uchokozi.Russia  imetoa mwito kwa wanachama wote wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa “kuepuka kuzidisha mvutano na kujiepusha na kushinikiza maazimio yanayozidisha mgawanyiko na uhasama.Msimamo wa Russia  unalingana na msimamo wa China, ambayo pia imekuwa ikipinga vikali miswada ya aina hii — ikiwemo ile iliyopendekezwa na Bahrain na kuungwa mkono na Marekani — na ambayo Russia na China zimeipinga kwa kutumia  kura ya turufu (veto). 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *